Nenda kwa yaliyomo

Msitu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msitu wa Kilimanjaro, nchini Tanzania.
Msitu mwingine.
Msitu wa Stara Planina, Serbia.
Msitu wa tropiki.

Msitu ni mkusanyiko wa uoto asilia unaojumuisha miti mingi ya aina mbalimbali (kwa mfano: mipingo, mikoko n.k.) mimea na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu.

Misitu inaweza kuwa za aina mbili:

  • ya asili au
  • ya kupandwa na binadamu (isiyo ya asili).

Misitu ya asili ni misitu ambayo huota yenyewe bila kupandwa na mwanadamu. Kwa mfano, msitu wa Udzungwa (Mkoa wa Morogoro, Tanzania) ni kivutio kikubwa cha watalii, hivyo kupitia msitu huu nchi inajipatia fedha za kigeni.

Misitu isiyo ya asili ni misitu ambayo hupandwa na mwanadamu kwa malengo mbalimbali.

Ndiyo tofauti kati ya misitu ya asili na isiyo ya asili.

Umuhimu wa misitu

Mara nyingi wanyama mbalimbali, wakubwa kwa wadogo, huishi na hutegemea uoto huo kwa kuwatimizia mahitaji yao kwa malazi na chakula.

Hata hivyo maisha ya binadamu hutegemea mazingira yake yanayomzunguka katika kujikimu kwani kupitia misitu mvua hunyesha na hivyo kusababisha ustawi na ongezeko la chakula.na kuepusha baa la njaa

Ni kwamba asilimia kubwa ya watu hutegemea kilimo ili kujipatia mahitaji yao ya kila siku, hasa katika nchi za Afrika ambazo ziko nyuma sana katika nyanja za utumiaji wa teknolojia za kisasa kama utumiaji wa zana za kilimo, k.mf. matrekta.plau,mashine za kuvunia mazao.

Hivyo katika kutimiza upatikanaji wa chakula kwa wingi ni lazima misitu ilindwe kwa nguvu zote katika ukuaji na ustawi wa jamii, la sivyo maisha ya viumbe vyote yatakuwa hatarini.

Majukumu kuhusu misitu

Tunatakiwa tutunze misitu kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe na vizazi vingine kwa sababu misitu inatusaidia kwa utalii na tunaweza kupata mvua kwa wingi.

Njia za kufuata katika utunzaji wa misituː

  • kupanda miti sehemu iliyokatwa miti
  • kupunguza kilimo cha kuhamahama
  • kuzuia uwindaji wa wanyama kwa kuchoma misitu
  • kuzuia ongezeko la watu katika eneo dogo
  • kuelimisha jamii juu ya utunzaji misitu

Faida za misitu ni:

  • Husaidia katika mfumo wa mvua
  • Hutumika kama makazi ya wanyama
  • Ni chanzo cha mapato ya nchi
  • Hutupatia dawa na chakula
  • hutupatia mbao kwaajili ya ujenzi

Hasara za ukataji mitiː

Hivyo ni muhimu kushauri watu watunze sana vyanzo vya asili kama misitu: hii ni kwa faida yetu wenyewe, inatusaidia hata kupata mvua kwa wingi.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msitu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.