Nenda kwa yaliyomo

Sputnik 1

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 21:25, 2 Oktoba 2017 na Kipala (majadiliano | michango) (Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Infobox Spacecraft | Name = Sputnik 1 | Image = 240px | Organization = Soviet Union | Major_Contracto...')
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Kigezo:Infobox Spacecraft

Sputnik 1 (Kirusi Спутник kwa maana msindikizaji) ilikuwa satelaiti ya kwanza iliyotengenezwa na binadamu iliyozunguka Dunia katika anga la nje. Ilitengenezwa katika Umoja wa Kisovyeti na kurushwa angani tarehe 4 Oktoba 1957 kutoka kituo cha Baikonur (leo nchini Kazakhstan). Sputnik 1 ilikuwa na umbo la tufe lenye kipenyo cha sentimita 58 na masi ya kilogramu 83.6. Ilikuwa na antena mbili zenye urefu wa mita 2.4 na 2.9. Ilibeba vifaa vya kupima jotoridi ndani yake pamoja na shinikizo ya gesi iliyojaa mwili wake halafu transmita ya redio iliyorusha vipimo hivi kupitia antena

Sputnik 1 ilizungukua Dunia mara 1,440 katika muda wa miezi 3 hadi kushuka na kuungua katika angahewa ya Dunia tarehe 4 January 1958.

Kurushwa kwa Sputnik 1 kulitokea wakati wa mashindano makali baina ya Umoja wa Kisoveti na Marekani. Marekani ilishtuka kabisa kwa sababu waliwahi kuamini ya kwamba walikuwa mbele. Mshtuko wa Sputnik ulisababisha mabadilio katika siasa ya Marekani iliyoongeza juhudi zake katika teknolojia na elimu. [1] Hapo yalianza mashindano ya anga (en:Space Race baina Marekani na Umoja wa Kisovyeti ambako pande zote ziliendelea kupeleka satelaiti nyingi kwenye anga zilizofuatwa na vyomboanga vya kubeba watu hadi Marekani ilifauli kufikisha watu mwezini mwaka 1969.


References

  1. Calmes, Jackie (2010-12-06). "Obama Calls for New 'Sputnik Moment'". The New York Times. Iliwekwa mnamo 2011-12-24.