Amri Kumi : Tofauti kati ya masahihisho
d roboti Nyongeza: diq:Des Emıri |
d roboti Nyongeza: am:አስርቱ ቃላት |
||
Mstari 137: | Mstari 137: | ||
[[af:Tien Gebooie]] |
[[af:Tien Gebooie]] |
||
[[am:አስርቱ ቃላት]] |
|||
[[ar:وصايا عشر]] |
[[ar:وصايا عشر]] |
||
[[arc:ܥܣܪܐ ܦܘܩܕܢܐ]] |
[[arc:ܥܣܪܐ ܦܘܩܕܢܐ]] |
Pitio la 21:41, 22 Februari 2011
Amri Kumi ni orodha za amri kuu za kidini katika Biblia.
Toleo la awali linapatikana katika kitabu cha Kutoka 20:1-17. Toleo la pili liko katika Kumbukumbu la Torati 5:1-21.
Amri hizi ni sehemu ya Torati ya Kiyahudi na kukubaliwa pia na Wakristo walio wengi kama amri zinazowahusu pia wao, tena kimsingi zinadai watu wote. Hata hivyo wafuasi wa Yesu Kristo wanazishika kadiri ya utimilifu wake ulioletwa kama Agano Jipya. Mifano ni mafundisho ya Yesu katika Injili ya Mathayo 5:17-48.
Maneno ya Amri Kumi
Maneno yanayojulikana kama “Amri Kumi” yanapatikana katika vitabu vya Biblia Kutoka na Kumbukumbu la Torati.
Kitabu cha Kutoka 20:2–17 | Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:6–21 |
---|---|
2. Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 3. Usiwe na miungu mingine ila mimi. |
6. Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 7. Usiwe na miungu mingine ila mimi. |
Mpangilio wa Amri Kumi
Maneno katika Kutoka 20 huwa na amri mbalimbali. Namba kumi ni hesabu iliyotiliwa baadaye kwa orodha hii haikuwa nia ya kiasili kuwa na amri “10” kamili. Ila tu tayari wakati wa Biblia ilikuwa kawaida kuziita "amri 10" lakini bila kuonyesha namba au mpangilio katika maneno ya Biblia yenyewe.
Hali hii ilisababisha tofauti ndogo katika hesabu ya amri hizi kati ya mapokeo ya madhehebu mbalimbali. Tofauti kuu ni kati ya Wayahudi wakifuatwa na Wakristo mbalimbali kwa upande moja na Wakatoliki pamoja na Walutheri na Wamoravian kwa upande mwingine kuhusu kutokuwa na sanamu za kuchonga. Tangu Agostino wa Hippo Wakatoliki walijumlisha sehemu kuhusu kutoabudu sanamu za kuchongwa pamoja na amri ya kutokuwa na miungu mingine. Kwa kufikia namba kumi Agostino aligawa sehemu ya mwisho kuwa amri mbili. Martin Luther alimfuata Agostino lakini Wareformed waliona mpangilio tofauti wakaihesabu kama amri ya pekee.
Amri | Wayahudi | Waanglikana, Wareformed na wengineo | Waorthodoksi | Wakatoliki, Walutheri, Wamoravian |
---|---|---|---|---|
Mimi ni Bwana Mungu wako | 1 | (utangulizi) | 1 | 1 |
Usiwe na miungu mingine ila mimi | 2 | 1 | ||
Usijifanyie sanamu ya kuchonga | 2 | 2 | ||
Usilitaje bure jina la Bwana | 3 | 3 | 3 | 2 |
Ikumbuke siku ya sabato uitakase | 4 | 4 | 4 | 3 |
Waheshimu baba yako na mama yako | 5 | 5 | 5 | 4 |
Usiue | 6 | 6 | 6 | 5 |
Usizini | 7 | 7 | 7 | 6 |
Usiibe | 8 | 8 | 8 | 7 |
Usishuhudie jirani yako uongo | 9 | 9 | 9 | 8 |
Usiitamani nyumba ya jirani yako Usitamani mke wake |
10 | 10 | 10 | 9 |
Usiitamani cho chote alicho nacho jirani yako | 10 |
Viungo vya Nje
- Maneno ya Amri Kumi katika Kutoka 20
- Maneno ya Amri Kumi katika Kumbukumbu la Torati 5
- Ulinganishaji wa matoleo ya Amri Kumi katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki, tafsiri ya Kiingereza, katika tovuti ya Vatikani. Katika kurasa zinazofuata kuna ufafanuzi mrefu wa amri hizo kwa jumla na mojamoja
Makala hii kuhusu mambo ya Agano la Kale bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amri Kumi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |