Ulaya : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
|||
Mstari 5: | Mstari 5: | ||
[[Picha:Grossgliederung Europas.png|thumb|300px|Kanda za Ulaya]] |
[[Picha:Grossgliederung Europas.png|thumb|300px|Kanda za Ulaya]] |
||
[[Picha:First.Crusade.Map.jpg|thumb|300px|Ulaya mwaka 1000 hivi]] |
[[Picha:First.Crusade.Map.jpg|thumb|300px|Ulaya mwaka 1000 hivi]] |
||
'''Ulaya''' (asili ya jina ni neno la [[Kiarabu]] ولاية, ''wilaayatun''<ref>Hivyo asili ya neno "Ulaya" ni sawa na "wilaya"; Krapf 1882 Swahili-English dictionary anaeleza: ""ULAYA (WALAYA au WILAYAya) ... mother-country in contradistinction to colonies, foreign possessions or parts"; Sacleux 1939 Dictionnaire Swahili-Francais anataja kama etimolojia ya Ulaya "Ar. Hind. ولاية wilaya, pays etranger" (=nchi ya kigeni) </ref>; inaitwa pia '''Uropa''') ni [[bara]] lenye eneo la [[km²]] 10,600,000 tu, lakini wakazi ni [[milioni]] |
'''Ulaya''' (asili ya jina ni neno la [[Kiarabu]] ولاية, ''wilaayatun''<ref>Hivyo asili ya neno "Ulaya" ni sawa na "wilaya"; Krapf 1882 Swahili-English dictionary anaeleza: ""ULAYA (WALAYA au WILAYAya) ... mother-country in contradistinction to colonies, foreign possessions or parts"; Sacleux 1939 Dictionnaire Swahili-Francais anataja kama etimolojia ya Ulaya "Ar. Hind. ولاية wilaya, pays etranger" (=nchi ya kigeni) </ref>; inaitwa pia '''Uropa''') ni [[bara]] lenye eneo la [[km²]] 10,600,000 tu, lakini wakazi ni [[milioni]] 699M Watu wa rangi tofauti na |
||
makabila.` |
|||
Wengi wenye asili ya Ulaya wakati wa [[ukoloni]] walitawanyika [[duniani]], hasa [[Amerika]], wakiathiri kote upande wa [[lugha]], [[utamaduni]] na [[dini]]. |
Wengi wenye asili ya Ulaya wakati wa [[ukoloni]] walitawanyika [[duniani]], hasa [[Amerika]], wakiathiri kote upande wa [[lugha]], [[utamaduni]] na [[dini]]. |
Pitio la 13:16, 28 Januari 2022
Ulaya (asili ya jina ni neno la Kiarabu ولاية, wilaayatun[1]; inaitwa pia Uropa) ni bara lenye eneo la km² 10,600,000 tu, lakini wakazi ni milioni 699M Watu wa rangi tofauti na makabila.`
Wengi wenye asili ya Ulaya wakati wa ukoloni walitawanyika duniani, hasa Amerika, wakiathiri kote upande wa lugha, utamaduni na dini.
Utawala
Katika karne ya 20, baada ya vita kuu mbili, nchi mbalimbali za Ulaya zilianza kushirikiana kwa njia mbalimbali:
- Baraza la Ulaya lina nchi wanachama 47
- Mkutano wa usalama na ushirikiano katika Ulaya (Marekani na Kanada ni wanachama pia)
- Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 28 tangu mwaka 2013.
Kanda za Ulaya
Katika orodha inayofuata kanda zinatajwa katika utaratibu wa Umoja wa Mataifa (UN categorisations/map). Lakini utaratibu huo haukubaliki ndani ya Ulaya kwa nchi za Ulaya ya Kati. Wajerumani, Waaustria, Waswisi, Wacheki, Waslovakia na Wapoland hukubaliana ya kwamba wenyewe si Ulaya ya Magharibi wala ya Mashariki ila Ulaya ya Kati. Kuna majadiliano kuhusu mipaka ya kanda hili yasiyokwisha bado, kwa mfano suala la Hungaria au Latvia.
Orodha ya nchi na maeneo
Jina la nchi au eneo, bendera |
Eneo (km²) |
Wakazi (mnamo Julai 2002 takriban) |
Wakazi kwa km² | Mji Mkuu |
---|---|---|---|---|
Belarus | 207,600 | 10,335,382 | 49.8 | Minsk |
Bulgaria | 110,910 | 7,621,337 | 68.7 | Sofia |
Ucheki | 78,866 | 10,256,760 | 130.1 | Praha |
Hungaria | 93,030 | 10,075,034 | 108.3 | Budapest |
Moldova | 33,843 | 4,434,547 | 131.0 | Kishineu |
Poland | 312,685 | 38,625,478 | 123.5 | Warshawa |
Romania | 238,391 | 21,698,181 | 91.0 | Bukarest |
Urusi (2) | 3,960,000 | 106,037,143 | 26.8 | Moscow |
Slovakia | 48,845 | 5,422,366 | 111.0 | Bratislava |
Ukraine | 603,700 | 48,396,470 | 80.2 | Kiev |
Denmark | 43,094 | 5,368,854 | 124.6 | Kopenhagen |
Estonia | 45,226 | 1,415,681 | 31.3 | Tallinn |
Visiwa vya Faroe (Denmark) | 1,399 | 46,011 | 32.9 | Tórshavn |
Finland | 337,030 | 5,183,545 | 15.4 | Helsinki |
Guernsey (3) | 78 | 64,587 | 828.0 | St Peter Port |
Iceland | 103,000 | 279,384 | 2.7 | Reykjavík |
Eire (Ireland ) | 70,280 | 3,883,159 | 55.3 | Dublin |
Kisiwa cha Man (3) | 572 | 73,873 | 129.1 | Douglas |
Jersey (3) | 116 | 89,775 | 773.9 | Saint Helier |
Latvia | 64,589 | 2,366,515 | 36.6 | Riga |
Lituanya | 65,200 | 3,601,138 | 55.2 | Vilnius |
Norwei | 324,220 | 4,525,116 | 14.0 | Oslo |
Visiwa vya Svalbard and Jan Mayen (Norway) |
62,049 | 2,868 | 0.046 | Longyearbyen |
Uswidi | 449,964 | 8,876,744 | 19.7 | Stockholm |
Uingereza (Ufalme wa Maungano) | 244,820 | 59,778,002 | 244.2 | London |
Albania | 28,748 | 3,544,841 | 123.3 | Tirana |
Andorra | 468 | 68,403 | 146.2 | Andorra la Vella |
Bosnia na Herzegovina | 51,129 | 3,964,388 | 77.5 | Sarayevo |
Kroatia | 56,542 | 4,390,751 | 77.7 | Zagreb |
Gibraltar (Uingereza) | 5.9 | 27,714 | 4,697.3 | Gibraltar |
Ugiriki | 131,940 | 10,645,343 | 80.7 | Athens |
Italia | 301,230 | 57,715,625 | 191.6 | Roma |
Masedonia Kaskazini | 25,333 | 2,054,800 | 81.1 | Skopje |
Malta | 316 | 397,499 | 1,257.9 | Valletta |
Montenegro | 316 | 397,499 | 1,257.9 | Podgorica |
Ureno (6) | 91,568 | 10,084,245 | 110.1 | Lisbon |
San Marino | 61 | 27,730 | 454.6 | San Marino |
Serbia | 102,173 | 10,280,000 | 100.6 | Belgrad |
Slovenia | 20,273 | 1,932,917 | 95.3 | Lyublyana |
Hispania (7) | 498,506 | 40,077,100 | 80.4 | Madrid |
Mji wa Vatikani | 0.44 | 900 | 2,045.5 | Mji wa Vatikani |
Austria | 83,858 | 8,169,929 | 97.4 | Vienna |
Ubelgiji | 30,510 | 10,274,595 | 336.8 | Brussels |
Ufaransa (8) | 547,030 | 59,765,983 | 109.3 | Paris |
Ujerumani (Udachi) | 357,021 | 83,251,851 | 233.2 | Berlin |
Liechtenstein | 160 | 32,842 | 205.3 | Vaduz |
Luxemburg | 2,586 | 448,569 | 173.5 | Luxemburg |
Monako | 1.95 | 31,987 | 16,403.6 | Monako |
Uholanzi (9) | 41,526 | 16,318,199 | 393.0 | Amsterdam, Den Haag |
Uswisi | 41,290 | 7,301,994 | 176.8 | Bern |
Armenia (10) | 29,800 | — | — | Yerevan |
Azerbaijan (11) | 39,730 | 4,198,491 | 105.7 | Baku |
Kupro (12) | 5,995 | 780,133 | 130.1 | Nikosia (Lefkosa) |
Georgia (13)} | 49,240 | 2,447,176 | 49.7 | Tbilisi |
Uturuki (14) | 24,378 | 11,044,932 | 453.1 | Ankara |
Kazakhstan (15) | 370,373 | 1,285,174 | 3.4 | Astana |
Total | 10,431,299 | 709,022,061 | 68.0 |
Tanbihi
1. Kanda zinazotajwa (Ulaya ya Kusini – magharibi n.k.) zinafuata utaratibu wa Umoja wa Mataifa UN categorisations/map. Nchi kadhaa zinazotajwa hapo chini zinaweza kuhesabiwa kuwa sehemu ya Ulaya na pia bara nyingine (Asia, Afrika, au Oceania). Hii inategemea na namna ya kugawa kontinenti; pia wakazi wenyewe wanaweza kujielewa tofauti na majirani yao.
2. Urusi ni nchi ya kontinenti mbili za Ulaya ya Mashariki na Asia; namba za wakazi na za eneo zimetasjwa kwa ajili ya sehemu ya Kiulaya pekee.
3–5. Guernsey, Kisiwa cha Man, and Jersey ni maeneo ya kujitegemea chini ya Taji la Ufalme wa Uingereza.
6. Namba za Ureno hazijumlishi Visiwa vya Madeira, ambazo ni sehemu ya Ureno magharibi ya Marokko katika Afrika.
7. Namba za Hispania hazijumlishi Visiwa vya Kanari magharibi ya Marokko katika Afrika, wa maeneo ya Ceuta na Melilla ambayo ni sehemu za Hispania kwenye pwani ya Moroko, Afrika ya Kaskazini.
8. Namba za Ufaransa hazijumlishi maeneo yake yaliyopo Amerika ya Kati au Kusini, Bahari Hindi au Oceania.
9. Uholanzi: Idadi ya wakazi ni ya 2004; Amsterdam ni Mji Mkuu lakini Den Haag ni makao makuuy a serikali.
10. Armenia huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki
11. Azerbaijan huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee.
12. Kupro huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Kusini; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu zisozo chini ya Dola ya Kituruki ya Cyprus.
13. Georgia huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee.
14. Uturuki ni nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Kusini; namba zinazotajwa zinahusiana na sehemu ndogo ya Magharibi pakee iliyomo Ulaya hasa jimbo lote la Istanbul.
15. Kazakhstan huhesabiwa mara nyingi kuwa nchi ya kimabara katika Asia ya Magharibi (kufuatana na kanda za UM) na Ulaya ya Mashariki; idadi ya wakazi na eneo zimetajwa za sehemu ya Ulaya pekee.
Tazama pia
Marejeo
- ↑ Hivyo asili ya neno "Ulaya" ni sawa na "wilaya"; Krapf 1882 Swahili-English dictionary anaeleza: ""ULAYA (WALAYA au WILAYAya) ... mother-country in contradistinction to colonies, foreign possessions or parts"; Sacleux 1939 Dictionnaire Swahili-Francais anataja kama etimolojia ya Ulaya "Ar. Hind. ولاية wilaya, pays etranger" (=nchi ya kigeni)