Mwalimu

(Elekezwa kutoka Walimu)

Mwalimu (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza teacher, school teacher na pengine educator) ni mtu anayesaidia wengine kupata ujuzi, maarifa na tunu.

Darasa la shule ya sekondari nchini Sierra Leone.
Mwalimu wa Kilatini na wanafunzi wake wawili, 1487

Kazi hiyo inaweza kufanywa na yeyote katika nafasi maalumu, kwa mfano mzazi au ndugu akimfundisha mtoto nyumbani, lakini kwa wengine ndiyo njia ya kupata riziki inayomdai karibu kila siku kwa miaka mingi, kwa mfano shuleni. Huko mwalimu anatakiwa kuwa na shahada au stashahada, kadiri ya sheria za nchi na ya ngazi ya elimu inayotolewa.

Imesemekana kuwa walimu vijana wanafundisha kuliko wanavyojua, yaani hata mengi wasiyoyajua vizuri. Wenye umri wa makamo wanafundisha yale yote wanayoyajua. Kumbe wazee wanafundisha yale yanayowafaa wasikilizaji.

Majukumu

hariri
 
Mwalimu wa shule ya msingi akiwa na wanafunzi wake matembezini, Colombia, 2014.

Majukumu ya mwalimu yanaweza kutofautiana kadiri ya utamaduni husika.[1][2]

Mara nyingi ni pamoja na kufundisha kusoma na kuandika, kuhesabu, kufanya kazi fulani ya mikono, kushirikiana katika jamii, kufuata dini, kuunda kazi za sanaa.

Kwa kawaida ufundishaji huo unadai mwalimu aandae somo kwa kufuata mtaala fulani, kutoa vipindi na kutathmini maendeleo ya mwanafunzi. Pia ni muhimu atunze nidhamu.

Nje ya madarasa, pengine mwalimu anatakiwa kuongoza wanafunzi wake katika safari za kutembelea mashamba, viwanda, kumbi, makumbusho, n.k.

Sifa zinazohitajika

hariri

Ualimu ni kazi ngumu sana, kwa sababu unahusika na mambo mengi.[3][4][5]

Umoja wa Ulaya umetaja sifa tatu muhimu:

Uwezo wa kushirikiana na wengine
Uwezo wa kutumia ujuzi, teknolojia na habari, na
Uwezo wa kufanya kazi ndani na pamoja na jamii.[6]

Wataalamu wa sayansi ya elimu wanazidi kukubaliana kwamba mwalimu yeyote anahitaji mambo matatu:

ujuzi (kufahamu mada na namna ya kuifundisha, mtaala, sayansi ya elimu, saikolojia, tathmini n.k.)
vipaji (kupanga kipindi, kutumia vifaa, kuongoza wanafunzi, kuendesha makundi, kutathmini maendeleo) na
misimamo (tunu, tabia, imani na uwajibikaji).[7]

Walimu maarufu

hariri

Tanbihi

hariri
  1. for a useful discussion see, for example: Cochran-Smith, M. (2006): 'Policy, Practice, and Politics in Teacher Education', Thousand Oaks, CA: Corwin Press
  2. see for example Cummings, W.K. (2003) 'The InstitutionS of Education. A Comparative Study of Educational Development in the Six Core Nations', Providence, MA: Symposium Books.
  3. For a review of literature on competences required by teachers, see F Caena (2011) 'Literature review: Teachers’ core competences: requirements and development' accessed January 2017 at http://ec.europa.eu/dgs/education_culture/repository/education/policy/strategic-framework/doc/teacher-competences_en.pdf
  4. F Caena (2011) 'Literature review: Teachers’ core competences: requirements and development' accessed January 2017 at http://ec.europa.eu/dgs/education_culture/repository/education/policy/strategic-framework/doc/teacher-competences_en.pdf citing Altet et al., 1996; Conway et al., 2010; Hansen, 2008; Seifert, 1999; Sockett, 2008
  5. 'Teachers Matter: Attracting, Developing and Retaining Effective Teachers', 2005, Paris: OECD publications [1]
  6. F Caena (2011) 'Literature review: Teachers’ core competences: requirements and development' accessed January 2017 at http://ec.europa.eu/dgs/education_culture/repository/education/policy/strategic-framework/doc/teacher-competences_en.pdf
  7. Williamson McDiarmid, G. & Clevenger-Bright M. (2008) 'Rethinking Teacher Capacity', in Cochran-Smith, M., Feiman-Nemser, S. & Mc Intyre, D. (Eds.). 'Handbook of Research on Teacher Education. Enduring questions in changing contexts'. New York/Abingdon: Routledge/Taylor & Francis cited in F Caena (2011)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwalimu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.