Muwa

(Elekezwa kutoka Miwa)
Muwa
(Saccharum spp.)
Miwa inayotoa maua
Miwa inayotoa maua
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo mnasaba na manyasi)
Nusufamilia: Panicoideae
Jenasi: Saccharum
L.
Spishi: Spishi zilizochaguliwa

S. arundinaceum Retz.
S. officinarum L.

Miwa (Saccharum spp.) ni aina za nyasi zinazotoa sukari.

Asili yake ilikuwa Asia ya Mashariki na kutoka huko zimesambazwa katika nchi za tropiki zenye mazingira yanayofaa kwake.

Kilimo cha mmea huo ni chanzo cha sehemu kubwa ya sukari kwa ajili ya matumizi ya binadamu na pia kwa sehemu kubwa ya ethanoli inayotengenzwa kwa matumizi ya biofueli.

Kwa ajili yake katika karne za nyuma ilistawi biashara ya watumwa hasa kutoka Afrika kwenda Amerika.

Kilimo

hariri

Muwa hulimwa kote katika nchi za kitropiki ukiwa ni chanzo cha asilimia 55 ya mahitaji ya sukari duniani. Nchi zinazolima muwa kwa wingi ni (uzalishaji wa mwaka 2005 kwa tani 1.000)

Nchi za Afrika ya Mashariki huzalisha kiasi kidogo tu duniani kama Tanzania (tani 300,000), Kenya (5,112,000) na Uganda (2,350,000).[1].

Kati ya mwaka 2004 na 2008 uzalishaji duniani uliongezeka kutoka tani bilioni 1.34 kufikia tani bilioni 1.74. [2]

Marejeo

hariri
  1. takwimu 2008 ya FAO http://faostat.fao.org/site/567/DesktopDefault.aspx?PageID=567#ancor Ilihifadhiwa 19 Juni 2012 kwenye Wayback Machine.
  2. takwimu ya FAO Food and Agriculture Organization of the United Nations (FAO) FAOSTAT - Production - Crops
  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muwa kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.