Liturujia ya Mesopotamia
Liturujia ya Mesopotamia ni liturujia maalumu yenye asili katika Mesopotamia ya kale, ambayo kimapokeo inatajwa kama imetokana na Mtume Thoma, na inatumiwa hasa na Wakristo Waashuru na Wakaldayo wa Iraq na nchi za kandokando, pamoja na Wamalabari wa India kusini, wengi wao wakiwa Wakatoliki na waliobaki Waorthodoksi wa Mashariki, ambao wote wametokana na wale waliotengwa na Mtaguso wa Efeso (431).[1][2] Kwa jumla ni milioni 5 hivi pamoja na wale waliotawanyika karibu duniani kote.
Hata matoleo ya vitabu vya liturujia hiyo kwa kiasi kikubwa yamefanywa na Wakatoliki. Lugha yake hasa ni Kiaramu.
Liturujia ya Kimungu
haririKuna anafora tatu: ya mitume Addai na Mari, ya Mar Nestori, na ya Mar Theodoro Mfafanuzi. Kati yake, ya kwanza ndiyo ya kawaida zaidi.
Yanafanyika masomo matano, manne au walau matatu, kutoka: (a) Torati; (b) Manabii, yaani vitabu vingine vya Agano la Kale; (c) Matendo ya Mitume; (d) Nyaraka za Mtume Paulo; (e) Injili. Mawili ya mwisho hayaachwi kamwe.
Kalenda
haririMwaka wa liturujia umegawanyika katika vipindi vya wiki sabasaba hivi, vinavyoitwa Shawu'i: Majilio (yanayoitwa Subara, "Kupashwa Habari"), Epifania, Kwaresima, Pasaka, Mitume, Joto, Elia na Msalaba, Musa na "Kutabaruku" (Qudash idta).
Tanbihi
haririViungo vya nje
hariri- "East Syrian Rite". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913. http://www.newadvent.org/cathen/14413a.htm.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Mesopotamia kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |