Pata mwenyeji mwenza anayekufaa kwenye Airbnb

Pata usaidizi wa hali ya juu, wa eneo husika kupitia Mtandao wa Wenyeji Wenza.
Na Airbnb tarehe 16 Okt 2024
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 16 Okt 2024

Sasa unaweza kupata na kuajiri mwenyeji mwenza kwa urahisi ili akusaidie kutunza nyumba yako na wageni, moja kwa moja kwenye programu.

Mtandao wa Wenyeji Wenza unakuunganisha na wenyeji wenza wakazi wenye ubora wa juu ambao hutoa usaidizi kulingana na mahitaji yako. Chagua kutoka kwenye orodha ya washirika watarajiwa, angalia uzoefu wao, anza kufanya kazi pamoja na ushiriki malipo yanayotumwa.

Mwenyeji mwenza anaweza kukaribisha wageni kwa niaba yako

Unaweza kuajiri mwenyeji mwenza ikiwa wewe ni mwenyeji mtarajiwa, mpya au mzoefu. Mwombe mwenyeji mwenza ashughulikie kazi mahususi au akaribishe wageni kwa niaba yako. Huduma zake zinaweza kujumuisha:

  • Kuandaa tangazo
  • Kuweka bei na upatikanaji
  • Usimamizi wa maombi ya kuweka nafasi
  • Ujumbe wa mgeni
  • Usaidizi wa mgeni kwenye eneo
  • Kufanya usafi na matengenezo
  • Upigaji picha wa nyumba
  • Usanifu wa ndani na mitindo
  • Vibali vya leseni na kukaribisha wageni

Wenyeji wenza wanaweza kuongeza huduma nyingine, kama vile mandhari, uchambuzi wa biashara na mafunzo ya ukarimu. Utapata maelezo kuhusu huduma ambazo mwenyeji mwenza hutoa kwenye wasifu wake.

Wenyeji wenza kwenye mtandao ni baadhi ya wenyeji wetu bora. Kwa wastani, wenyeji wenza wana ukadiriaji wa jumla wa nyota 4.86 kutoka kwa wageni na uzoefu wa miaka minne kwenye Airbnb. Leo, asilimia 73 ni Wenyeji Bingwa na asilimia 84 wanakaribisha wageni kwenye angalau nyumba moja ambayo ni Kipendwa cha Wageni.

Mtandao wa Wenyeji Wenza kwa sasa unapatikana nchini Australia, Brazili, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Meksiko, Uhispania, Uingereza na Marekani. Mtandao huu utaenea kwa nchi zaidi mwaka 2025.

Ni rahisi kutumia Mtandao wa Wenyeji Wenza

Tumia Mtandao wa Wenyeji Wenza kutafuta na kuungana na mtu anayetoa huduma unazohitaji.

Tafuta mwenyeji mwenza:

  • Weka anwani ya nyumba yako ili utafute mtandao wa mtu aliye karibu. Utaona wasifu wa wenyeji wenza wakazi, walioorodheshwa kulingana na mambo kama vile eneo, ushiriki na ubora.
  • Chagua wasifu wa mwenyeji mwenza ili upate maelezo zaidi kumhusu, uzoefu wake, tathmini zake za zamani, matangazo anayokaribisha wageni, bei na maelezo mengine.
  • Tuma ujumbe kwa kila mmoja wa machaguo yako makuu. Jitambulishe na utoe maelezo machache kuhusu mahitaji yako.
  • Fikiria kuuliza maswali ya ziada na ujadili matarajio yako ya kukaribisha wageni.

Ajiri mwenyeji mwenza:

  • Amua ni nani ungependa awe mwenyeji mwenza na ufikirie kuweka maelezo ya ushirikiano wako katika makubaliano rasmi.
  • Nenda kwenye tangazo lako kwenye Airbnb. Mtumie mshirika wako mpya mwaliko wa kushirikiana kukaribisha wageni na uweke ruhusa zake kwa ajili ya tangazo lako. Atakuwa na wiki mbili za kukubali.
  • Chagua kushiriki sehemu ya malipo unayotumiwa kwa kila nafasi inayowekwa kupitia Airbnb.*

Zana zote unazohitaji ili kushirikiana na mwenyeji mwenza ziko katika programu. Unaweza:

  • Kumtumia ujumbe mwenyeji mwenza moja kwa moja.
  • Kumwalika akaribishe wageni kwenye tangazo lako.
  • Kuweka ruhusa zake za kusimamia tangazo lako.
  • Kushiriki na mwenyeji mwenza wako malipo kwenye nafasi zilizowekwa.*

*Baadhi ya masharti yanatumika, kulingana na eneo la mwenyeji, mwenyeji mwenza na tangazo.

Mtandao wa Wenyeji Wenza unapatikana nchini Ufaransa, Uhispania, Italia, Ujerumani, Uingereza, Australia, Meksiko (unaendeshwa na Airbnb Global Services Limited), Kanada, Marekani (unaendeshwa na Airbnb Living LLC) na Brazili (unaendeshwa na Airbnb Plataforma Digital Ltda).

Wenyeji kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza kwa kawaida wana ukadiriaji wa juu, viwango vya chini vya kughairi na uzoefu thabiti wa kukaribisha wageni kwenye Airbnb. Ukadiriaji unategemea tathmini za wageni kwa matangazo wanayokaribisha wageni au kushirikiana kukaribisha wageni na huenda usiwakilishe huduma za kipekee za mwenyeji mwenza.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
16 Okt 2024
Ilikuwa na manufaa?